"Siwezi Kuacha Muziki, Ni Malezi Tu"Stara Thomas
Msanii wa muziki wa kipya katika mahadhi Zouk, Stara Thomas ameamua kuweka wazi kuwa kimya chake kilitokana na kutingwa na malezi ya watoto wake.Stara aliyasema hayo hivi karibuni wakati akilonga na Dar411 baada ya baadhi ya wadau kulalamika kutomsikia kwa muda mrefu huku wengine wakisema huenda akawa ameacha muziki."Siwezi kuacha muziki,siyo tu unanipatia riziki, bali pia upo katika damu, sema ndio hivyo kwamba ukibanwa inabidi ufanye na vitu vingine, lakini kuacha siyo rahisi" alisema."Malezi ndugu yangu,asikuambie mtu, kulea watoto ni kazi ngumu sana,inakunyima nafasi ya kutoka muda unaotaka na kufanya mambo yako vyema."Lakini sasa baada ya kuwa na umri unawaruhusu kukaa peke yao bila kuhitaji uangalizi wa karibu kutoka kwa mama narejea tena kwenye fani,".Alisema kwa sasa anajiandaa kutoa kazi yake mpya ambayo hata hivyo bado hajaipa jina kwa kuwa bado naimalizia...na atakuwa kwenye position ya kutaja jina lake mara tu utakapokamilika.Stara Thomas, mmoja kati ya wasanii wa kike anayeheshimika na aliye fanya vyema katika fani hiyo kwa muda mrefu, amekuwa kimya kiasi cha kudhaniwa kuwa ameachana na kazi hiyo.Source: www.dar411.com
No comments:
Post a Comment