Thursday, 22 March 2007

Jamani...Jamani..Mguu Huo?
Kwa wale watunguaji wenzangu wazuri napenda kuwapa umiza kichwa hapo pichani ili ujiulize swali moja wabunifu wanafikiri nini kama hiyo Driving Moc inayotengenezwa na Brox Brand ambacho kwa wale watu wa milipuko nadhani kwa kukiona tu wameshapangia mpaka mavazi rasmi ya kulipuka nacho bila wasiwasi,na wala sina haja ya kuwaeleza zaidi ila ukitaka kutungua mdundo huo unahitaji kuwa na kama box $130 hivi ili upewe na risiti kwamba umekitungua rasmi.....sina la kusema vitendo tu!Aiseee huu mdundo balaa!

No comments: