Wednesday, 21 March 2007

Lime!



Lime ndo ndimu jamani, sasa ipo rangi ya ndimu haswaa ile ndimu ambayo haijaiva ndo rangi ambayo imetufungulia mwaka huu katika rangi kama ilivyokuwa rangi pink mwaka jana. Najua utakuwa umepishana wajanja wameitinga au kuona madukani vitu viingi vikiwa vimegubikwa na hii rangi kama pochi, tops, heren, sketi , skafu na viatu pamoja na pamba kibao za kike na mashati pia ya kiume. Rangi hii nakumbuka enzi silee nipo shule ya msingi ilikujaga lakini tulikuwa tunaziita crazt color kutokana na mng’ao wake, na zilikuwa rangi mbili kama ilivyo lime na hii rangi ya machungwa maarufu kwa sasa kama Bambucha!! Haya mabinti ili ufanane na mjanja na uende na wakati huna budi ya kusaka kivazi kama sio viatu , pochi au chochote upendacho ili kabati lako lifanane na wenzio wanaoenda na fashion. Hata wewe kaisake mtu wangu!!

1 comment:

Anonymous said...

Rangi naifagilia hii imetulia sana, inamkubali mtu yeyote hasa ukimachisha koti, pochi na viatu