Friday, 30 March 2007

Sandals ”malapa” zilivyopanda chati!!




Hata sijang’amua kiswahili cha Sandals maana nilihoji malapa na ndala kama zaweza kuwa sandals, wajuzi wa mambo wameniambia helll Noooo haziwezi itwa sandals sababu wengi hutumia kuogea yaani malapa na ndala hazina hadhi ya sandols Anyway wacha nami niite sandals tu sababu nia yangu ni kuzingumzia hizi sandols ambazo zimemwagika kibao madukani yaani ni toleo jipya kwa kina dada sasa wanazivaa sehemu yoyote ile , yaani imepewa hadhi ya kiatu cha kufunika ambavyo wengine wanadiriki kutokea out au kuvalia hata na suti mradi tu iwe na turangi twa kumechisha na nguo,pochi au hata mapambo. Kwa mtaji huo tunaweza ona shanga zinavyopata deal na wale wanaouza viatu vya sandols vyenye shanga wanasema hivyo ndivyo vina deal kwa sasa mradi tu upangilie rangi vizuri. Madesigner kama LV, Gucci,burberry nawengineo kibao nao hawako nyuma wameshazimwaga sokoni sandals zikiwa zimerembwa kwa rangi tofauti na urembo wa vito vya kung’aa (stones)pamoja na chata zao...kama kawa Enzi hizo viatu kama hivyo vilikuwa vya kushindia nyumbani au kuendea dukani (kuwepo around) lakini sasa watu wanapuyangia town na kutinga navyo hata kwenye mtoko wa maana kama hawana akili nzuri Si unajua kuna hotel au club fulani haziruhusu kuingia na sandals, lakini kwa sasa wamechemsha kwani ndio viatu vyenyewe vya kuulambia kwa kina dada, si wajua huwezi bishana na fasheni kama huizimii unaipisha inapita lakini inakuwa ipo ipo tu!!

No comments: