Tuesday, 27 March 2007

Simple Mtoko!

Hii ni spesho kwa warembo wote wanaopenda kulipuka pamba kali na simple wakati wowote,Nadhani kama uonavyo pichani ni mambo ya style za kisasa kabisa za mabinti wapevu wa milipuko ya mavazi na huo ni mfano 2 wa jinsi gani unaweza ukaamua kutoka bomba mbaya hata kuliko Beyonce,yeye amejilipua na office kubwa {miwani} na kijiblauzi simple kenye nakshi kidogo,kaptula white na simple flat sendoz kali za gold.Sasa hapo mmekubali style inazidi kukuwa na watu wanazidi kuvaa simple na kutoka bomba mbaya!Au nimekosea ?

1 comment:

Anonymous said...

beyonce katoka funky sana. ningewashauri hawa dada zetu waki bongo kuvaa vitu kama alivyovaa beyonce kutokana na joto iliyopo bongo!