Tuesday, 12 June 2007

Akon....Jamaa Anajua Kuirepresent Afrika Kinoma....



Huyo ndio mwanamziki mahiri sana kutoka Barani Afrika (Akon) ambaye makazi yake yako Marekani na kwa kusema ukweli jamaa anawikilisha vizuri sana na kujitangaza vyema asili ya kiafrika na kwa ujumla bara la afrika...kwasasa huyu jamaa ni hot cake kinoma huko kiwanja kwa kipaji chake cha kuimba,utungaji mashairi na pia uproducer wa nyimbo mbalimbali....na kwale ambao hawajapata taarifa basi jamaa kutokana na kukubalika kwake na kipaji alichonacho ndio kimefanya kukubalika na hivi majuzi kala kimeo cha kutengeneza album mpya ya Whitney Houston ....basi turudi kwenye mada yetu unaonaje jamaa anavyovaa simple na kwa ukaribu tazama pichani utaona t-shirt lake jinsi lilivyoandikwa kwamba "Beliave In The Future Of Africa"na ni kweli kabisa kwakuwa jamaa anatumia ufamous wake kuelezea hisia zake kwamba kwa watu watoe fikra potofu kwamba afrika hatuna mwelekeo....Big Up sana Akon kwa kurepresent vyema Afrika......na umelipuka simple na umetoka bunduki kinoma.....

1 comment:

DERRICK MUSHOBOZI said...

Sheria kama jamaa kala kimeo cha kutengeneza albam ya Whitney houston basi jamaa ni noma ile kichizi halafu kwenye suala la pamba katoka ndukii nyc and simple nimependa hayo maanadishi BELIVE IN THE FUTURE OF AFRICA.