Wednesday 29 October 2008

MIRIAM ODEMBA AINGIA TANO BORA KATIKA SHINDANO LA VAZI LA TAIFA

miriam katika vazi la taifa
miriam akitangazwa kushika nafasi katika tano bora
miriam akiwa na washindi wenzie wa tano bora
miriam akimeremeta na washindi wenzie
***********************
Na washindi ni kama wafuatao:
1. Panama
2.Philippines
3. Columbia
4. Tanzania
5. Greece
Mashindano ya Vazi la Taifa ya Miss Earth 2008 yalifanyika jana usiku (tarehe 28 Oktoba 2008) katika ukumbi wa PAGCOR jijini Paranque, nchini Ufilipino.
Warembo 85 walishiriki katika mashindano haya na Miss Panama alishinda tuzo kuu la Vazi bora la Taifa.Miss Philippines alishinda tuzo la Miss Photogenic na tuzo mbalimbali maalum zilitolewa na wadhamini katika mashindano haya.Miss Greece alipata tuzo 2 maalum - Miss Micu Confidence and Joel Cruz Signature Award,.Miss Aficionado ilinyakuliwa na mrembo wa Tanzania - Miriam Odemba, ambapo Miss Venezuela alishinda tuzo la Face of Placentana tuzo la Face of the Night lilikwenda kwa Miss Colombia.
Vazi la Miriam Odemba lilibuniwa na mbunifu mahiri na mzoefu wa Zanzibar Farouque Abdela na limetayarishwa kwa kutumia mifuko ya plastiki na kunakshiwa na mikufu ya kimasai.
Fainali ya Miss Earth yatafanyika tarehe 9 Novemba 2008.
Habari Kwa Hisani Ya Michuzi

1 comment:

Anonymous said...

wish u all the best ms odemba