Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency ambayo ni waandaji wa Mashindano ya Miss Tanzania Hasheem Lundenga amesema Tanzania inakusudua kutuma maombi ya kuandaa mashindano ya urembo ya dunia.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashim Lundenga, alisema hivi karibuni kuwa, wamepanga kutuma ujumbe maalumu jijini Laondon, Uingereza yalipo makao makuu ya waandaaji wa shindano hilo.
Lundenga alisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa wanaweza kufanya hivyo, hatua ambayo pia iliungwa mkono na wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
“Tumekuwa na wazo hilo la kuandaa mashindano kwa muda mrefu baada ya kuona tuna uwezo huo, lakini tumepata nguvu zaidi baada ya wadhamini wetu (vodacom) kukubaliana na wazo letu hilo”, alisema Lundenga.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa wanajua itachukua muda mrefu mpaka maombi yao kukubaliwa kutokana na sera za waandaaji wa Miss World kutotabirika imebidi watume ujumbe hilo kisha kusubiri hatima yao.
Aliongeza kuwa mchakato wa Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano ya dunia unaonyesha utakuwa mrefu kutokana na shindano hilo kufanyika mara nyingi zaidi katika nchi za Bara la Afrika, tofauti na mabara mengine.
Baadhi ya nchi hizo ni pamoja na Afrika Kusini ambayo imeandaa shindano hilo zaidi ya mara tano tangu kuanza kwa mashindano hayo mwaka 1954.
Source:dar411.com
No comments:
Post a Comment