Usiku wa Khanga za Kale
Usiku wa jana katika ukumbi wa Diamond lilifanyika onyesho la khanga za kale lililoandaliwa na mbunifu maarufu Tanzania Asia Idarous.
Katika onyesho hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mh Sophia Simba lilianza kwenye majira ya saa nne usiku ambapo walipita warembo wengi tofauti tofauti kuonyesha aina mbali mbali za mavazi yaliyotengenezwa kwa kutumia khanga.
Zaidi ya hilo waliweza kupanda wasanii mbali mbali kusindikiza onyesho hilo, kilikuwepo kikundi cha taarabu kutoka Zanzibar cha Zanzibar Morden Taarab, Malkia wa mipasho Khadija Kopa nae alikuwepo, Deo Mwanambilimbi pia alikuwepo.
Kivutio kikubwa ni pale ilipoonyeshwa khanga aliyotumia mwanaharakati wa zamani Bibi Titi ambapo iliweza kushangiliwa kwa nguvu mara ilipotangazwa kupita.
Kwa ujumla shindano liliweza kufana sana.
Onyesho hilo liliandaliwa na Fabak Fashion chini ya udhamini wa Clouds FM na Kipindi cha Leo tena.
Kwa picha na kilichojiri zaidi katika onyesho hilo bofya Hapa

Source: www.dar411.com
No comments:
Post a Comment