Friday 27 July 2007

Nature kufunga ndoa August!

Hatimaye msanii Juma Kassim Nature anatarajia kuongeza idadi ya wasanii wanaokimbia genge la makapera hivi karibuni.Kwa mujibu wa Nature,anatarajia kufunga ndoa August 18 na mpenzi wake wa siku nyingi aliyemtaja kwa jina la Pili.Harusi hilo litafanyika (Shy-Town) Shinyanga ambapo ndipo nyumbani kwa mpenzi wake huyo.Safi sana nature na kila la kheri.....

1 comment:

DERRICK MUSHOBOZI said...

Kila la heri Juma nature katika kukamilisha mipango yako ya harusi ndugu yangu na mungu akubariki uwe mume mzuri kwa mkeo mtarajiwa