Friday, 13 July 2007

TID Aburuzwa Mahakamani!

Msanii Khalid Mohamed 'TID',jana aliburuzwa (Mahakamani) ya kinondoni akikabiliwa na mashtaka ya kum-muvuzishia makonde na kumjeruhi raia mwema.Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Benedict Nyagabona, alidai kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 2 mwaka huu, saa 6.30 usiku, katika hoteli ya Slipway jijini.


Ilidaiwa kuwa msanii huyo alimtwanga Ben Mashiba, kwa kono lake la kushoto na baada ya hapo kumtupia ‘ashtrei’ kichwani, ambayo ilimjeruhi na kumsababishia maumivu mazito.Hata hivyo TID alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana hadi July 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.Hakimu wa kesi hiyo alitaja masharti ya dhamana kuwa ni wadhamini wawili wanaofanya kazi katika ofisi zinazotambulika.Tarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea,TID alipewa siku tano za kumaliza suala hilo na mgomvi wake, lakini alishindwa kufanya hivyo na ndipo alipoburuzwa kwa Pilato.

No comments: