Monday 30 July 2007

Wema Sepetu avunja rekodi!!

Kwa kashfa ukilinganisha na warembo waliopita ambao walishika taji katika kinyang'ayiro cha Miss Tanzania tangu mwaka 1994Akiongea jijini Hashimu Lundenga mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania alidai kuwa Wema amezidi ukimlinganisha na warembo wengine waliopita kwani hakuna mrembo aliyewahi kuwa na kashfa kama yeye...Ndio habari zingine zinaweza zikawa si za kweli lakini ndo zimeandikwa na pia ni mrembo ambaye tumemuonya kwa barua ajirekebishe mwenendo wake....alisema LundengaWema amekuwa mremo wa kwanza kuandikwa kwa kashfa nyingi zaidi hususan za ngono ukimlinganisha na warembo wengine waliowahi kushika taji hilo.Na Lundenga aliwataka warembo wote watakaojitokeza katika shindano la Miss Tanzania mwaka huu kujiheshimu na kuachana na tabia zisizofaa kwani huharibu sifa na heshima ya kamati nzima.

1 comment:

Faith S Hilary said...

Well...maybe she wasnt sure if she was a role model 4 other girls in da country but she ruined herself..used 2 b in da same xul but she was never der..actually after she was miss tanzania but i think she will change...it's candy1