Monday 6 August 2007

Filamu ya Amina Kuandaliwa

Aliyekuwa mbunge wa Vijana kupitia tiketi ya CCM,Viti Maalumu, Marehemu Amina Chifupa ameandaliwa filamu itakayoonyesha maisha yake mpaka kufikia mauti.Muandaaji wa filamu hiyo Kulwa Kikumba 'Dide' alisema wameamua kuandaa filamu hiyo kutokana na baadhi ya wasanii kuwa karibu na mbunge huyo.Dide alisema mbali na hilo, pia itaonyesha baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo na wadau wa nchini na hata nje watakao onekana kutoa nasaha zao juu ya yale aliyoyafanya na kusisitiza marehemu Amina Chifupa.Aliwataja baadhi ya wadau watakaoonekana kwenye filamu hiyo kuwa ni Fina Mango, Dinna Marios, Maimatha, Miss Tanzania 2006-07 Wema Sepetu, Nancy Sumari, na aliyekuwa Miss Tanzania 2005-06.Pia alimalizia kwa kuwataja wasanii watakao shiriki katika filamu hiyo kuwa ni Steven Kanumba pamoja na Sinta.

No comments: