TBL yatoka na tuzo ubunifu
Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Redd's Premium imeibuka na tuzo ya ubunifu wa mavazi ya Kiafrika.Mashindano hayo ya ubunifu yamezinduliwa rasmi Hotel ya Sea Cliff jijini Dar na mshindi wa kwanza ataweza kujishindia dola za Marekani $5000.Meneja wa kinywaji hicho Mpeli Nsekela alisema kuwa mshindi vilevile atazawadiwa tiketi ya kwenda Afrika Kusini kuhudhuria maonesho ya mavazi.Kwa kuanzia washiriki watachora picha ya mavazi yanayoendana na staili za Kiafrika na zitachaguliwa picha 10 katika hizo zitakazotengenezewa nguo kama zinavyoonekana.Mashindano hayo yana nia ya kuibua vipaji vya wabunifu wadogo wanaochipukia
No comments:
Post a Comment