Majina ya wanaowania Tuzo za Vinara kutajwa Alhamis!
Na Mwandishi Wetu
Majina ya wasanii na filamu zilizoingia katia hatua ya mwisho ya kuwania Tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania (Vinara Film Award) 2007-2008 yanatarajiwa kutolewa Alhamis ya Mei 22 mwaka huu ikiwa ni baada ya kumalizika kwa kazi ya kupitia filamu zilizoingizwa kuwania tuzo hizo.
Jopo la majaji lililofanya kazi hiyo kwa wiki tatu huku wiki ya mwisho wakifanya kazi usiku na mchana ili kumaliza kazi hiyo Jumapili ya Mei 18, 2008 kama ilivyopangwa, wanatazamiwa kutaja majina matano kwa kila tuzo itakayowaniwa.
Kwa mujibu wa msemaji One Game Promotions inayotoa tuzo hizo, Bi Khadija Khalili, jopo hilo linatarajiwa kutangaza majina hayo katika mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika siku hiyo ambapo majina matano yatatajwa kwa kila tuzo inayowaniwa.
"Jumapili ya Mei 18 mwaka huu, majaji wetu walikamilisha kazi hii ya kusaka majina matano-matano kwa kila tuzo inayowaniwa... Wakati wa mashabiki kushika pumzi zao umewadia, kwa kujua nani kaingia na nani katoka," akasema.
Bi Khalili alisema kuwa, baada ya kutangazwa rasmi kwa majina hayo, mshindi wa kila tuzo atatangazwa siku ya onesho la utolewaji wa tuzo hizo litakalofanyika Ijumaa ya Mei 30, mwaka huu katika ukumbi utakaotangazwa baadaye.
Tuzo za Vinara wa Filamu nchini zitatolewa kwa mara ya kwanza nchini kwa lengo la kutoa changamoto kwa fani hiyo kama ilivyokuwa kwa fani karibu nyingine zote nchini ambazo kila mwaka hupatikana washindi.
Tuzo hizo zimedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt, Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), 88.4 Clouds FM, Free Media, Digital Art, Club Scorpion, Global Publishers, Kiu Investment, Wamasa Publications na Regency Park Hotel.
Msemaji huyo alisema kuwa, zaidi ya filamu sabini za Kitanzania zimewasilishwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu.

No comments:
Post a Comment