Wednesday, 26 November 2008

Miriam Odemba
Miriam Odemba akionesha Crown yake original kabisa aliovishwa mara baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya Miss Earth Air 2008 yaliyofanyika nchini Filpine hivi karibuni

Miriam akiwa amepozi na waheshimiwa usiku huu ndani ya hoteli ya Newa Africa,katika hafla ya kumpongeza mlimbwende huyo.kati ni baba yake mzazi Miriam Odemba pamoja na Prof Philimon Sarungi
Miriam akiwa amepozi na wageni waalikwa mbalimbali usiku huu ndani ya new africa hotel waliofika kumpongeza
Mkurugenzi wa Kampuni ya Campass Communication Maria Sarungi akizungumza mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya kumpongeza mlimbwende wa Dunia namba 2 Miriam Odemba baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya miss Earth yaliyofanyika hivi karibuni nchini Ufilipino. Hafla hii imefanyika usiku huu ndani ya hoteli ya New Africa.Maria Sarungi alisema kuwa Odemba bado ana kazi kubwa inamkabiri mbele yake kuhakikisha taji hilo linabaki kwa Tanzania, kama vile haitoshi ameongeza kuwa Odemba pia atashiriki kufanya kazi mbali mbali za kijamii hapa nyumbani na pia desemba 28 atarejea nchini Filpine kuungana na mshindi wa kwanza katika kufanya kazi za kijamii nchini humo.Pia atatembelea nchi mbalimbali ikiwepo Singapore na nyinginezo.Aidha Maria amebainisha kuwa Miriam amepata mkataba wa mwaka mmoja wa kufanya kazi nchini humo
Picha na Maelezo Kwa Hisani Ya Michuzi Jr

No comments: