Friday, 19 March 2010

Balozi wa India Nchini Tanzania Mh. K.V Bagirath (wa pili shoto) akiwa katika picha ya pamoja na Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika usiku majuzi nyumbani kwa balozi Oysterbay jijini Dar. Richa Adhia anaondoka jumapili kwenda nchini Afrika Kusini kushiriki kwenye shindano la Miss India Worldwide litalofanyika katika jiji la Durban Machi 27. Hii ni mara ya kwanza kwa Mtanzania mwenye asili ya india kushiriki katika shindano hilo lililoanzishwa mwaka 1990. Pili kulia ni mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali na mfanyabiashara mashuhuri jijini Dar, Kiltda Patel.
Balozi wa India Nchini Mh. K.V Bhagirath (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Samsung Miss Tanzanian India (wa tatu kushoto) pamoja na maafisa wengine wa ubalozi wa India nchini na waratibu wa Samsung Miss Tanzania India pamoja na wageni waalikwa katika hafla ya kumuaga mrembo huyo iliyofanyika nyumbani kwa balozi. Oysterbay jijini Dar usiku ma juzi.
Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia Aagwa Rasmi Jana

2 comments:

Anonymous said...

Mustapha Hassanali looks like he can collapse anytime! Someone get him a drip of vitamins, proteins and some cholesterol! Kafanyiwa stomach bypass surgery au ni nini hicho?

Anonymous said...

jamani nilidhani peke yangu mbona nuru ya uhai imetoka? anaumwa au ndo diet. Nooo jamani msaidieni jamani noooo bado tunamhitaji