

Mwisho Mwampamba akipokea shada la maua kutoka kwa ndugu zake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jana jioni akitokea Afrika kusini kwa ndege ya shirika la ndege la SAA ambako alishiriki shindano la BBA 2010 All Stars na kushika nafasi ya 4 huku mshiriki Uti kutoka Nigeria akijinyakulia kitita cha Dola laki mbili za Kimarekani.
Mwisho kesho anatarajiwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari na kueleza mambo mbalimbali yaliyojiri kwa muda wote wa miezi mitatu walipokuwa kwenye jumba la Bigbrother na washiriki wenzake na keshokutwa atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika picha kwanza juu ni baba yake mzee Mwampamba.
Picha ya pili akiwa ndugu zake pamoja na walinzi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jana jioni akitokea nchini Afrika Kusini alikoshiriki katika shindano la BBA 2010 All Stars na kushika nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment