Fashion hizi zitatufanya tuonekane machizi,
Miaka ya karibuni ulikua ukionekana umetinga mavazi yenye urembo wa kung’aa au meremeta wakati wa mchana ulikua unaonekana mshamba wa kuja. Tofauti na siku hizi ukitinga kivazi chenye urembo wa kung’aa unaonekana mjanja tena unaenda na wakati. Kama kawa wanamitindo wanahamasisha kuzalisha bidhaa zenye ungaro hususani wa silver na gold. Usishangae ukiwa unakatiza mitaani ukapishana na mrembo katinga kipochi au kavaa viatu vyenye rangi ya dhahabu au fedha na mkanda kiunoni ili kubalance (kumechisha). Utaona top ”blauzi” au bazee limedariziwa kwa urembo wa dhahabu pamoja na fedha. Ili kuungana na wajanja usisite kuinunua ukipishana nayo wakati wa shopping. Its all about styles au sio jamani!!
1 comment:
you cant go agaist the trendy... whats in is in... no one can fight it... not just gold n silver, people kill the colour with red, we acha tu!
Post a Comment