Empire Design lebo inayobanana na Wakati!!!!!
Bongo kwa sasa kumekuwa na wabunifu luluki ambao wanabuni mavazi na wengine tayari wana lebo ambazo wameanza kuzitambulisha, moja kati ya hizo lebo ni EMPIRE DESIGN.
Lebo ambayo inamilikiwa na Mwanadada anayeenda kwa jina la Rahma Mwapachu . Yeye kaanza kwa kutengeneza tops kwa ajili ya kina dada na t-shirt kwa ajili ya kina kaka ambapo pamba hizo amevibatiza majina tofauti wazungu husema ’Brand’ Kama IM BONGOLICIUOS ambapo mi niliianza kuiona nikajua labda ndo lebo yenyewe ,sio siri nilipagawa si unajua sie ndo wazalendo wenyewe hatuna budi kujivunia ubongo wetu!! Nilikutana na Rahma akaniambia la hasha hii sio lebo bali ni moja kati ya majina ambayo yapo chini ya lebo ya Empira , na si hiyo tu bali kuna Maji Baridi,Jogoo, Good Girl ,African Queen ,Vote 2005 na Empire yenyewe. ....unajua nimeweka majina tofauti hivi ili nisichoshe wateja wangu, na ninatoa jina kulingana na wakati mfano kwa sasa hivi tukiwa tunaelekea kwenda katika uchaguzi ndo maana nimetoa Vote 2005, najua wengi watapenda kuvaa hii ili kuhamasisha uchaguzi bei ni rahisi kila mtu anaweza kuafford ni alfu 10-15........alisema Rahma Alisema watu wana kawaida ya kuchukia kitu kikiwepo kiiingi nae amegundua hilo ndo maana ana brand nyiingi ambazo anatoa chache kulingana na wakati huo na jina lenyewe. Haya wabongo Empire ndo hiyo iko mtaani ikiwa na brand luluki , bila shaka imekupagawisha zinapatikana mtaani au kwa maelezo zaidi cheki nao Email empiredesigns@gmail.com au namba ya simu 255 744 285168 kwa mauzo ya jumla na rejareja.
No comments:
Post a Comment