Friday, 27 April 2007

Mchakamchaka Wa Shaggy Alipotumbuiza Bongo!

Pichani ni Mwanamziki Maarufu Duniani Shaggy siku alipowarusha wabongo mchakamchaka pale Diamond Jubilee....Nadhani watu wengi mnamkubali sana huyu jamaa kwa style yake ya mavazi na kwa kifupi style zake zinamtoa kinoma..kama hapo pichani alilipuka mnyuko mmoja wa kukata na shoka...Pensi la Army,Adidas White All Star,White Longsleeve,Blazer la Grey lenye viraka nyuma ya mikono black na Kofia (kapelo) ya grey na mistari white...kusema ukweli alitoka baruti bovu siku hiyo...ila mnawaona na wabongo hawakuwa nyuma siku hiyo pia nadhani ukiangalia hii picha utatathimini pamba nyepesi zilivyokuwa zinawakilisha nadhani hata Shaggy alishtuka kuona watu wanavyojilipua bongo....Big Up sana wabongo kwa ubishi nawakubali mnoo...

1 comment:

DERRICK MUSHOBOZI said...

Jamaa napenda sana anavyovaa simple haweki madude kibao mwilini huwa siku zote anatoka simple tshirt jeans na simple shoes namkubali vilivyo kama ilivyo hapo pichani ametoka kiushkaji sana ambayo stayle hiyo inaweza kuwa pia imekamata vilivyo