Thursday, 5 April 2007

Alimaarufu Kama Grosgrain Belt!
Aina hii ya mikanda simple sana na iliyokaa kama utambi.Na wenzetu wanapenda kuziita aina hizi za mikanda kwa ujumla kama Grosgrain Belt...... na kwa huo pichani unaitwa Striped Grosgrain Belt kwasababu ya mistari iliyopita....Nadhani kila mmoja wetu anajua inapendezaga sana kwenye suruali za aina ya cadet au khaki na hata kwenye pensi ama kaptula na kwa kumalizia kabisa ukitaka unaweza kujilipua hata kwenye jeans pia....nadhani mmenisoma hapo!

6 comments:

DERRICK MUSHOBOZI said...

Hii mikanda ilivyo juu sasa hivi ukigusa bei yake nayo iku juu lakini kama unavyosema mzee mkanda kama huo unafaa sana kwenye jeans na ukilipuka nao kwenye pensi pia fresh unatoka bomba sana mambo ya GROSGRAIN BELT hayo halafu upate kitu chenye strips kama hicho unafunika ile mbaya.
Mzee mzima wa sheria na mavazi hapo nimekusoma mtu wangu aminiaaa....

Sheria Ngowi. said...

nashukuru sana mdau wangu derrick kama umenisoma hapo...nadhani tupo pamoja hapo?hehee

Anonymous said...

Ok ok ok!!...hapo vimesemwa vitu ambavyo unaweza kuvaa na hiyo belt hapo..lakini vyote vilivyosemwa ni ''Bottoms''...vipi kuhusu ''Tops''...yaani...what colour looks good with that...!?!?!

Anonymous said...

I like the belt...je unaweza kuvaa kama ''Tibaigana Style'' ?

Sheria Ngowi. said...

kusema ukweli mdau wangu hutaweza kuvalia kama mikanda ya tibaigana kwakuwa hii mikanda ni membamba sana na pili ni kwajili kuvalia ndani ya suruali,kaptula hata jeanz!

Sheria Ngowi. said...

nadhani tops za rangi nyeupe na blue zitatoka nyoko sana na vile vile tops ndogondogo au t-shirts ndogo ndogo zinapendeza inategemeana na rangi ya aina ya mikanda hiyo ndivyo utatakiwa kumatch kunatokana na rangi zilivyo itapendeza mdau wangu...nadhani umenipata hapo