Hongera Sana Taifa Starz...Pia Naomba Kuuliza Swala?

Napenda kuipa hongera sana timu yetu ya Taifa Stars (Serengeti Boyz) kwa kuliwakilisha vyema Taifa letu vizuri huko Burkina faso na kurudi na ushindi mzuri na pia nisisahau kutuma salama zangu za pongezi kwa mapokezi mazuri waliyoandaliwa na watanzania wenzetu pale nyumbani kwa kuwapa mapokezi ya kihistoria na serekali yetu kushiriki kwa hali na mali na kwa moyo mmoja kuwapa heshima kubwa sana kwa ujio wao waliporejea nyumbani jana...lakini nilikuwa na swali la 1:nilikuwa nataka kupata maoni yenu watanzania wenzangu na wadau zangu popote pale mlipo ni kuhusu swala la jezi za timu yetu ya taifa kuwa na chata ya adidas nilitaka kujua ni kwamba hiyo brand kwasasa hivi ndio wadhamini wao wakubwa?ama wanavaa 2ili mradi wamevaa?maanake kama wanavaa tu bila kuwa na mkataba wowote na hiyo kampuni sio sawa kabisa kwakuwa kama wanavaa tu hiyo chata bila malipo yoyote si sawa maanake wanakuwa wanaifanyia biashara hiyo kampuni bila kulipwa chochote ambalo kwangu mimi binafsi ni makosa makubwa sana ni heri hata jezi zetu zingetengenezwa au kubuniwa na wabunifu wa pale nyumbani na kuwa na nembo ya mbunifu husika kuliko kuweka chata hiyo ya adidas wakati hawalipwi chochote...swali la 2:je kwanini wachezaji wa timu yetu ya taifa hawako in formal outfit kama timu za wenzetu wanavyovaa? kama suti za maana pale wanapokuwa katika safari zao za kwenda kuliwakilisha taifa popote pale duniani au hata wakiwa katika dhifa yoyote waendako?nadhani ni lazima wangepatia suti zilizodesigniwa mahususi kwaajili ya timu ya timu hiyo kama embu tazameni pichani kusema ukweli si sawa kwa wao kwenda sehemu kubwa kama bungeni wakiwa wamevaa majezi tu au track suit ni aibu sana au mnasemaje wadau zangu?ingetakiwa hao wafadhili wawafikirie kwa hilo na pia hata jezi wadesign zilizokuwa na hadhi nzuri tofauti na wanazovaa sasa?chama cha mpira fat na wafadhili wote wanaoifadhilia timu yetu wawasaidie hata kwenye mavazi kama suti za maana,jezi zenye hadhi ya juu na hata kuwe na mabasi makubwa na maalum kwa timu yetu ya taifa?jamani hamuoni timu za wenzetu sio tu za nje tutazame za hapa hapa barani ketu afrika kama Timu za bafana bafana (south afrika),Senegal,Cameroon n.k wanavyovaa na kuwekwa kwenye hadhi ya juu? kumbukeni popote wanapoenda timu kama yetu wanaliwakilsha taifa letu na kutuletea heshima kubwa sio lazima waende wakiwa katika hadhi ya hali ya juu sana ila lazima wawe nadhifu sana,nadhani mtakubaliana na mimi wadau zangu kuwa Mfano:ukimuona mtu kavaa fresh popote pale ni vigumu sana kujua undani wake kwakuwa uvaaji wake nadhifu ndio unamficha kasoro zake alizonazo ndio hivyo hivyo tufanye kwa timu yetu ya taifa kwakuwa ndio inachipua katika ulimwengu wa soka na kuwa maarufu kwahiyo basi hata kama tunaitwa maskini tusikubali na dhana hiyo kabisa kwakuwa sio kila kitu tuonekane maskini au tuko chini kivile ...hayo ni maoni yangu tu niliyoona nishare na nyie wadau zangu na watanzania wenzangu popote pae walipo kwa mafanikio mazuri ya taifa letu kwa ujumla na timu yetu ya taifa....Pics @ www.issamichuzi.blogspot.com.
.....
1 comment:
Style hii inabidi tujifunze sababu wachezaji hawawzi kuingia kienyeji tu wakiwa na jeans na jezi juu nafikir kwa mtazamo wangu ingekuwa vizuri zaidi wangekuwa na suti it would have looked nice halafu pia hilo loo ya addidas sidhani kama wanalipwa na pia kama wao adiddas wana idea.Mtazamo wangu ni kwamba awepo mtu ambaye atasimama kama designer wa timu ya taifa kuanzia jezi hadi suti za wachezaji hizo hela zote zilizotolewa na wafadhili sidhani kama watashindwa kutoa milipni tano kuwashonea suti za maana lazima tuwe na tendence hata kama ikiwa wachezaji watabadilishwa kwenye timu ya taifa hizo funds zote zinazotolewa na wafadhili sidhani kama watu watashindwa kushonewa suti lazima tufanye mambo kwa uhakika tusifanye mambo ya kienyeji wenzetu timu zao za taifa sehemu kama hizo huwa wanaingia wamevaa suti sababu ni sehemu maalumu tusijifanye maskini kiasi hicho kwamba hatuwezi ku-afford hata suti kama tunaweza kuwapa motisha wachezaji wetu inayofikia milioni 30 kila mmoja kwanini tushindwe kuwapa suti za kwenye hafla maalumu hili nawaachia wadau wenyewe nafikiri watalichukua kwa uzito na pia kujitahidi kuwasiliana na madesigner mbali mbali.
Post a Comment