
Asubuhi ya Tarehe 26 itakuwa ni siku ya Tanzania kuandika Historia kwenye mchezo wa mpira wa kikapu pale mchezaji anayetamba toka chuo cha Connecticut (UConn) Hasheem Thabit atakapokuwepo kwenye ule uchaguzi wa wachezaji wanaotoka chuo kwenda kwenye ligi hiyo maarufu ya kulipwa duniani NBA.
NBA Draft inatarajiwa kuchezeshwa kuanzia muda wa saa moja asubuhi za Afrika Mashariki siku ya tarehe 26 (CAT) kwenye ukumbi wa Madison Square Garden.
Hasheem ambaye ni mmoja wa wachezaji waliotamba kwenye ligi ya vyuo kwa mwaka jana kwa wastani wa pointi 14 na rebound 11, Hasheem Thabit alichaguliwa kuwa mchezaji mshiriki bora wa mwaka 2008-2009 na pia alitangazwa kuwa mlinzi bora wa mwaka 2008-2009 kwa mara ya pili mfululizo.
All The Best Hasheem!

1 comment:
Good Luck Boy
Post a Comment