Thursday, 25 June 2009

TID Anusa Jela Tena

Mwanamuziki Khalid Mohamed a.k.a TID anaonekana kuinyatia tena Jela baada ya kumshambulia Binti mmoja Naima Abdalah kwa kumpiga kwenye Club ya Thai Village iliyopo pande za Masaki.

Chanzo chetu cha Uhakika kinasema TID alifanya tukio hilo la kusikitisha kutokana na kutoelewana kati yake na mrembo huyo ambaye inasemekana ni mwanafunzi wa shule moja jijini Dar es Salaam.

“Chanzo ni kutoelewana baina ya TID na Naima sasa sijui ni nini zaidi, ila watu tulishudia zogo kubwa kiasi cha jamaa kutolewa nje na mabaunsa, na inasemekana Naima kashachukuwa RB kwa ajili ya kumkamata TID” kilisema chanzo chetu.

Kama TID atakutwa na makosa hayo tena basi kuna uwezekano mkubwa wa kutupwa jela kwa mara ya pili ndani ya mwaka mmoja, kwani ni mwaka jana tu jamaa ndio katoka jela alikokuwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa msamaha wa Rais.

Inasemekana Mama mzazi wa TID baada ya kugundua hilo alimwaga chozi kutokana na kumuonea huruma mtoto wake kwa vitendo vyake.

Source: www.dar411.com

No comments: