Thursday, 10 May 2007

Brown N' Yellow Zinapomix Zinakuwa Hivi!

Nadhani wadau zangu wengi mmeshajaribu pindi mkiwa mnajipigilia kuvaa rangi za Brown N' Yellow na nadhani majibu yake kila mmoja wetu anayafahamu vizuri ni jinsi gani zinareflect bomba sana...kama hapo pichani juu ni Marques Huston akiwa amelipuka sweater la yellow,shatindani la brown,blazer lenye rangi ya brown na mistari ya njano na chini kamalizia na jeans ya fedout blue ambayo kusema ukweli amependeza sana na hiyo miwani mikubwa yenye frame ya nyeusi na vioo vya light and dark brown kwa pamoja.Nadhani pia mmemsoma mrembo wake pembeni alivyojinyuka gauni hilo simple ila lenye mapindo pindo yanalolifanya gauni hilo kuzidi kuwa na style ya kipekee...nadhani wakuu mmesoma hisabati nzima hapo pichani....kazi kwenu


1 comment:

DERRICK MUSHOBOZI said...

Nimelikubali koti la Marques Houston