Wednesday, 2 May 2007

Interior Designing!

Mnaonaje Sitting Room Yako Ikiwa Simple Namna Hiyo.......

Nataka kuuliza swali moja wadau zangu...hivi mnaonaje nyumba zetu pale bongo zingekuwa zinadesigniwa katika hali ya kuweka vitu simple ndani na nyumba kuwa simpla na unique kama uonavyo hapo pichani...tatizo ni nini hasa?Ni kukosa material...wabunifu wa ndani (interior designers) au ni kuogopa gharama kufanya hivyo?maanake najua zipo baadhi ya nyumba pale bongo zimedesigniwa fresh sana kwa nje ila ukiingia ndani ni tofauti kabisa na muonekano wa nyumba nje.....kwa mimi naona nyumba ikiwa simple ni uamuzi wa mtu husika wala sio gharama wala nini kwakuwa naamini mtu ukiwa na choice nzuri unaweza ukaweka vitu simple na vya gharama nafuu na nyumba ikatoka bomba kinoma....mwonekano wa nje sio muhimu sana kwangu ila ndani naona ndio muhimu sana au uongo wadau wangu?

1 comment:

DERRICK MUSHOBOZI said...

All i can say it simple and clean vitu vichache halafu quality,ingekuwa bongo hapo kungekuwa na stuli si chini ya tano kabati kubwa halafu limejazwa madude kibao hadi mtu kupita unapita kiupandepande halafu sofa zingekuwa kama seti mbili zimejazwa vitambaa inabidi wabongo tujifunze kuwa kujuza vitu kibao sitting room sio ujanja