Friday, 13 July 2007

Banana Zorro Ala Kimeo!

Msanii maarufu na mahiri kwa miondoko lainiii ya Bongo Flava,Banana Zorro..amekula bingo ya kufa mtu baada ya kuchaguliwa na kampuni kubwa la simu za mkononi duniani la Motorolla...kuwa balozi (Motorolla Ambassador) wao kwa hapa nchini.

Banana ambaye pia anamiliki bendi ya B-Band...ameangukiwa na mtende huo hivi karibuni na tayari amekwisha anza kuuza sura kwenye matangazo mbalimbali ya simu hizo ktk magazeti mbalimbali hapa Bongo.Sasa naona mambo yanakwenda shwari kabisa kwa wasanii wetu hayo ndio tunaita maendeleo taratibu ndivyo yanavyoanza...mnasemaje wadau zangu imetulia hiyo nadhani kwa ujumla na big u sana Banana endelea huo ndio mwendo mdungo.....

2 comments:

Anonymous said...

Sheria, kwani kimeo maana yake nini? pengine mie naelewa tofauti

Sheria Ngowi. said...

kula kimeo maanake ni kupata dili flani faster...mdau wangu hapo juu