Tuesday, 24 July 2007

Jamani,Jamani,TID tena!

Sijui tuite ni mkosi au balaa kwa msanii huyu,lakini ukweli ni kwamba...msanii TID ambaye songi lake la 'Nyota Yako' limebamba kinoma kiasi cha kung'ang'ania kwenye Top Ten za Radio na Tv kadhaa hapa East Africa...amekumbwa na zahma kubwa ambalo asipoangalia anaweza kupotea kwenye ulimwengu wa muziki.Nasema hivyo kwasababu imebainika kuwa songi lake hilo la 'Nyota Yako'..limeibwa kila kitu kuanzia beat mpaka mashairi,kutoka kwa msanii mmoja wa Mozambique.Kwa mujibu wa kituo cha Radio One kilichofanya mahojiano ya moja kwa moja na msanii huyo kutoka Mozambique,kazi hiyo ya TID inafanana kila kitu na kazi yake aliyoitoa miaka mitatu iliyopita lakini akiwa ameimba kwa lugha ya kwao.Hata hivyo TID alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema yeye hajui lolote kuhusu nyimbo hiyo kwani songi hilo pamoja na mashairi yake aliuziwa na Producer wake Said Comorien.Sasa basi kasheshe ni kwamba msanii huyo kutoka msumbiji inaelezwa yuko njiani kuja nchini ambapo hatujui anakuja kuchukua hatua gani...kwa ujumla naweza kusema kisa kizima kama kitamhusu TID au Producer wake Said Comorien na kama wizi huo utathibitishwa basi watakuwa wametutia aibu ya ajabu.Je kwa maoni yako ni nani tumwazibu kati ya hawa!

2 comments:

DERRICK MUSHOBOZI said...

Mkuu ilo soo nimelisikia tena kwa masikio yangu tena hapo hapo radio one kuhusiana na sakata la hio nyimbo kiukweli hasa ni kwamba nyimbo hiyo ya NYOTA YANGU ya TID inafanana na ya huyo jamaa wa msumbiji kila kitu kuanzia mashairi hadi melody na huyo jamaa ni kweli kwamba aliuimba sababu hata ukipigwa redioni unafanana kila na wa TID na huo wimbo wa huyo jamaa wa msumbiji unaitwa NYOTA YANGU ambao ni sawa na wa TID kwa lugha ya kiswahili kitu amabcho kimenifanya nijiulize imekuwaje nyimbo zifanane kuanzia melody,chorus hadi mashairi tunafahamu kuwa wasanii wanaweza kukubaliana kwa kupewa haki ya kuimba nyimbo ya mwenzako lakini kwa upande mwingine yeye said comorien yeye anasema alishawahi kwenda huko na kuimba nyimbo kama hiyo na kuiacha huko sasa sijui msema kweli ni nani lakini pamoja na yote hayo inawezekana kwa namna moja au nyingine TID anajua au hajui kuwa wakati anapewa hiyo nyimbo prodyuza wake alikuwa ameitoa mahali fulani na kama ni mchezo wameufanya waangalie sana maana kitakachotokea hapo huyu jamaa kutoka msumbiji anaweza kuwa sue hawa jamaa kwa hela nyingi sana kitu ambacho kitakuwa kimemuharibia TID vibaya sana pamoja na said comorien ila hapo wakulaumiwa nafikir itakuwa ni prodyuza kama matamshi anayosema ni ya kweli kuwa alipewa kila kitu na prodyuza wake lakini kama ni soo pia TID lazima litampitia sababu naye kaimba nyimbo ambayo siyo ya kwake.

Anonymous said...

Yeah, but he can come out of copyright infringement by talking to the original artist, ofcourse the original artist may decide he wants payment but these newspaper people are making it bigger than it is!!All he has to say is I loved your song and I didn't know how to reach you so I'm sorry but he can compensate as easy as that!!