Wednesday 25 July 2007

Kazi ya Tajiri wa Sauti!!

Wakati mikakati ya kuanzisha bendi yake ikiwa inaendelea vizuri,Abubakar Shaaban Katwila ’Q-Chillah' amekamilisha albam yake ya nne iitwayo `Tajiri wa Sauti` itakayoingia mtaani wakati wowote kuanzia sasa.

Ikiwa imesheheni nyimbo kali zenye kila aina burudani kama alivyojigamba mwenyewe...itakuja ikiwa imeshirikisha vichwa vikali Afrika Mashariki akiwemo Jose Chamelione, Princess Sheila wa Uganda na wengineo. Miongoni mwa track zilizomo katika albam hiyo ni pamoja na unaotamba hivi sasa katika vituo mbalimbali vya radio wa `Nakupenda` ambao ameuimba kwa lugha tatu Kiingereza, Kiganda na Kiswahili akishirikiana na mwanadada Sheila.

No comments: