Thursday, 2 August 2007

Big Brother Africa Yanarudi Tena!

Bila shaka majina ya wafuatao Mwisho Mwampamba (Tanzania), Gaitano Kagwa (Kenya), Cherise Makabela (Zambia), waliweza kujipatia umaarufu mkubwa katika Bara la Afrika kutokana na kushiriki shindano lililokuwa likifahamika kama Big Brother Afrika.Katika shindano hilo la Big Brother Afrika, Cherise ndiye aliyeibuka kinara na kufuatiwa na Mwisho na kufuatiwa na Warona, kwani ilikuwa ni mwaka 2003.

Kwa sasa kaa mkao wa kula na Big Brother nyingine iliyoshirikisha washiriki 12, watafungiwa katika jumba moja kwa siku 98 za kuwania kitita cha dola 100,000 kama zawadi atakaye ibuka kinara.Kama ilivyo ada ya mashindano yote ya Big Brother Africa (BBA), washiriki hao watakuwa wakienguliwa mmoja mmoja kila wiki na hatimaye kumpata wa mwisho atakaye tangazwa kama mshindi na kujinyakulia zawadi hiyo.Haya sasa kaa tayari kwa ajili ya uhondo huo kutoka kwa washiriki, ambao kila mmoja atakuwa na wakati mgumu wa kuonyesha uwezo wake ili aendelee kuwamo katika jumba hilo, na linatarajia kuanza Jumapili ijayo ambapo wapenzi na mashabiki wa shindano hilo watapata fursa ya kutazama matukio yote kupitia Televisheni zao.Kipindi hicho kitaonyesha uhalisi wa mambo halisi kutoka kwa washiriki, kitazinduliwa Jumapili ijayo huko Johannesburg.

No comments: