Monday 27 August 2007

Skuli kwisha,sasa makamuzi!

Baada ya kujichimbia takriban miaka mitatu akisaka nondo kwenye chuo cha MSTCDC huko A-Town (Arusha),gwiji la miondoko ya Zouk,Paul Mbena..almaarufu kwa jina la 'Mr Paul'...anarejea upya akiwa albam mpya kwapani.Msanii huyo aliyewahi kutamba na songi nyingi tu za kimahaba......aliweka wazi kuwa albam lake hilo jipya liitwalo 'Asante Sana' litakuwa na nyimbo nane...na kwamba litatinga kwenye market wakati wowote kuanzia now.Kwa mujibu wa Paul,nyimbo karibu zote zipo kwenye mahadhi ya Zouk...kasoro moja iitwayo 'Nakupenda' iliyo kwenye mahadhi ya Kwaito na ambayo amempa shavu mwanadada Stara Thomas.Albam nzima ni kazi ya studio za Metro za jijini Dar es Salaam

No comments: