Monday 27 August 2007

Sweety kwenye maandalizi!

Baada ya singo yake 'Walimwengu si Wazuri' kumtendea vyema masikioni mwa watu,mwanadada Nuru Magram..a.k.a Sweety,ameonekana kunogewa na sasa anajipanga ili aweze kurelease singo nyingine ambayo anaamini itamng'arisha zaidi.

Hayo aliyasema ktk mahojiano ya hivi karibuni na kudai kuwa mpaka sasa bado hajajuwa atoke na songi jipi...kwani zote alizonazo anaziamini kuwa ni motooo.Akiendelea anasema kibao chochote atakachochomoka nacho kitakuwa kimetoka ndani ya albam yake yenye songi 10 aliyoipa jina la 'Walimwengu'.Katika albam hiyo kutakuwa na mchanganyiko wa miondoko ya Zouk pamoja na Reggae.

No comments: