Friday, 19 October 2007

R.I.P LUCKY DUBE!

Mwanamziki wa mtindo wa reggae kutoka Afrika Kusini, Lucky Dube , ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi usiku wa kuamkia jana huko katika kitongoji cha Rosettenville, Johannesburg nchini Afrika Kusini.Polisi wa jijini Johanesburg wanasema majambazi hao walikusudia kuliiba gari la mwanamziki huyo.Lucky Dube alikuwa amerekodi zaidi ya Album ishirini na kuzuru karibu pembe zote duniani akiimba nyimbo zenye ujumbe wa kijamii . Watanzania watamkumbuka kwa ziara kadhaa alizowahi kufanya nchini Tanzania na pia muziki wake uliokuwa na ujumbe wa amani na kimapinduzi.R.I.P LUCKY DUBE...AMEN.

No comments: