Monday, 19 March 2007

Pensi Nyanya.....Gaucho....Kapri


Najua wengine mwasoma hii huku mnafurahia!! najua nimewakumbusha mbali sana ,mabinti warembo mpo pamoja na hili kwani pensi nyanya kwa sasa ipo mtaani na imebatizwa jina la Gaucho Ni aina ya pensi ambayo ipo katika material ya fulana ambayo mengi ni mafupi hadi magotini wakati baadhi ni marefu hadi chini Nayo yapatikana ya kila rangi huku mengine yakiwa yamenakshiwa na urembo wa kudariziwa au vito vya rangi mbali mbali..hakika yanapendeza, Naomba niongezee na style hii ambayo wataalam wanaiita ’Kapri’ ni kaptura fupi na za kubana ambazo zimepindwa chini au kupasuliwa pembeni katika kuweka nakshi,nazo zipo katika fashion usije ona ukashangaa Nyingi zinaishia juu ya magoti,nazo unazikuta katika rangi tofauti,katika material ya vitambaa vya suruali na hata jeans...mmenisoma nadhani!

No comments: