Ni lebo mpya ya nguo ndani ya Bongo ambayo wamiliki wameiweka kwenye Hip Hop Gear,wakimaanisha ni mavazi ya kisanii ya Hip Hop. Wamiliki wa lebo hiyo 120 ambao ni kampuni ya 120 Entertainment , ambao pia wanaandaa event,wana Boze Cruz, pamoja na kupromote wasanii. Akiongelea pamba hizo ambazo wasanii pamoja na wazalendo kibao wanatinga, mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dagma Iddi alisema si pamba tu bali kuna stika za kwenye magari pia.
...kuna tops, t-shirt na suruali t- shirt na kila aina ya kunguo pamoja na kofia zitakuja hv karibun ....alisema Dagma na kusema bei za pamba zao ni bei poa yeyote anaweza vaa akipenda. malighafi wananunua Asia na china then wanazitengeneza katika kiwanda kilichopo jijini pamoja nakuweka lebo yao ya 120.....speed 120 ya gari na wenyewe wanakwambia ndo speed ya maisha kila mtu atakiwe aende mwendo huo wa maisha kuna wapenzi wa DHW ambao wako nje ya nchi tayari wameanza kuagiza stika na hizi pamba kutoka kwa marafiki na ndugu zao wakidai wanaona fahari kutinga lebo ya home, na hii yaonyesha malengo ya vijana hawa kuipanua hii lebo afrika mashariki na kisha dunia nzima itatimia. kama umeizikia wanakwambia cheeki nao dagmar120@hotmail.com
No comments:
Post a Comment