Masofa na vitambaa vya kufuma ...wapi na wapi!!
Leo nimeona nihamie mambo ya Interior Designing kwani tumeng’ang’ania saana vitu vingine kuliko tunapoishi au mnasemaje wadau?Warembo naongea na nyie sababu ninauhakika nyie ndo warembaji nyumba unapeleka proposal ikiitishwa ndo mr anafanya mambo ya invoice uongo?? haya turudi kwenye mada, siku hizi naona furniture centers nyingi zimemwagika na aina tofauti za sofa zinauzwa kuna sofa za ngozi na hata zile za vitambaa lakini yenye material ya sofa nyingine zikiwa za rangi moja na nyingine zikiwa na maua ua urembo tu wa aina tofauti sasa pale warembo ukiwa nalo lile sio lazima upachike vitambaa vyako vya kufuma jamani au hata kama vitambaa redmade lakini usiweke kwenye hizi sofa, Ndo maana twaenda na wakati vitambaa vyako vile uvirembe kwenye yale makochi yetu ya mbao na mito ya sponch kwa wenye kuyangangania mpaka sasa. Kwani haya ya sasa tayari yanaurembo wake ndo maana mwaona mchongo wake imerembwa, au aina ya kitambaa tayari imesharembwa ina maua au tangi zimepangiliwa kati ya mito ya kitambaa na sofa zenyewe....hapo kitambaa kina nafasi badili ya kitambaa ukitaka kulihamasisha (kulipendezesha) basi tupia tumito twa umbo tofauti kopa, kisu na duara au vyovyote basi mjengo utakuwa umelipuka swafi kabisa na utakamata Big Up kibao......Sasa mjipange tunaambiana tu au sio.....!
No comments:
Post a Comment