Thursday, 5 April 2007

Swali......Ni Sababu Ya Pesa Au Choice Pia Inachangia?

Swali nililokuwa nataka kuwauliza moja tu wadau zangu ambalo linanipa utata mkubwa labda mawazo yenu ndio yanaweza kunifanya nijue ukweli...Hivi kama Oprah uvaaji wake unatokana na pesa mingi aliyonayo ndio analipuka pamba kali namna hiyo au pia ana choice nzuri ya kuchagua mavazi mazuri pia inachangia kwa kiasi kikubwa hata bila kuangalia mshiko kiasi gani anao?maanake anajilipua na pamba kali sana ?je jibu ni pesa alizonazo ama choice nzuri aliyonayo ndio inampelekea anavaa vizuri namna hiyo?

3 comments:

DERRICK MUSHOBOZI said...

Mimi kwa mtazamo wangu mzee wa sheria na mavazi huyu mama OPRAH kwanza hela anayo pia pamba anazifahamu vizuri kama utakuwa na kumbukumbu nzuri huyu mama amefunika mara nyingi kwenye masuala ya mavazi hasa anapohudhuria hafla kubwa kubwa kama vile GOLDEN GLOBE AWARDS na nyinginezo nyingi kifupi ni kwamba hela anayo halafu na pamba pia anajua jinsi ya kuzipangilia vilivyo yaani huyu mama ni amejaliwa vitu vyote hivyo viwili hapo nimemuaminia kila kitu amesimama ile mbaya pia na hela aliyonayo inachangia sana kulipuka vitu vyenye utata maana inaonekana kwenye choice ya nguo amesimama ile mbaya nhope umenipata hapo mzee mzima wa sheria na mavazi

Sheria Ngowi. said...

hapo nimekusoma kamanda ni kweli kabisa ulivyosema mama natisha sana!

Anonymous said...

mimi naona sababu sio pesa..kwasababu hata ukiangalia kwenye talk show yake..jinsi anavyovaa, anaenda na mwili(shepu) wake na rangi anazochagua pia zinampendeza..kwahiyo kusema ukweli ni choice yake