Friday, 30 March 2007
Culture Zimepamba Moto Tena....
Mtindo wa uvaazi mavazi yenye ubunifu mahiri wa culture za kiafrica kwasasa umerudi tena kwa kasi kubwa mno na hii imechangiwa sana na mitindo ya rasta ambayo kwa % kubwa bongo watu wameamua kuweka na inawatoa poa sana.....kama uoavyo Mwanamziki Mahiri Wa Kughani Bongo...Sir Juma Nature wakiwa kwenye mazungumzo na Jose Chamillione na kwa nyuma anaonekana Dazi Baba na Richie......nadhani kama unavyo pichani Sir Nature katoka poa sana na Culture Style aliyovaaa ya aina ya Jah......Jamani nyumbani ni nyumbani tu style zimerudi tena masela!

Lowcut Kwa Warembo!
Kuanzia zamani mtindo wa warembo kunyoa nywele fupi kama wanaume ulikuwapo miaka hiyo kabla ya mlipuko wa kuweka dawa za nywele kama relax,kalikiti n.k.Lakini kwasasa warembo wengi wanakata nywele zao kurudia ile style ya zamani nawatoka bomba mbaya kama uonavyo pichani ila sheria kubwa ni kwamba inategemeana na kichwa na kichwa cha mrembo.....manasemaje hapo mabinti?

Nani Zaidi Kati Wanamziki Hawa...... RAY-C Vs K-LYNN ......Kwa Kulipuka Pamba?
Ray-C
K-lynn

Ndugu wadau zangu wa blogu hii nilikuwa naomba maoni yenu kuhusu nani mkali katika kulipuka pamba kali kati ya Wanamziki Mahiri Wa Bongo Fleva Bongo kati ya wabinti warembo Ray c Vs K-lynn?naombaeni maoni yenu wadau?........kazi kwenu....
Mapochi..Blauzi Za Vidotidoti...Shanga Shingoni...Viko Hot!
Tunaanza kwa kuongelea swala la kurejea kwa mapochi makubwa kama style ya kisasa...kumbuka vilikuwapo tangia zamani ila wakati huu vinapendeza sana kutokana na ubunifu wake wa hali ya juu sana....hata pia viblauzi au magauni yenye vidotidoti pia ni style kali kinoma kwa sasa na watu wanajilipua nayo na bila kusahau shanga za shingoni ambavyo kwa wenzetu mtoni ni vitu wanavidhamini tokea zamani kuvivaa na hasahasa watu matajiri ila shanga zao zinakuwa ni madini ya lulu au pearl......pichani Miss Tanzania 2005 Nancy Sumari akiwa katika mlipuko huo mkali......wabinti mmenisoma hapo?

Sandals ”malapa” zilivyopanda chati!!

Hata sijang’amua kiswahili cha Sandals maana nilihoji malapa na ndala kama zaweza kuwa sandals, wajuzi wa mambo wameniambia helll Noooo haziwezi itwa sandals sababu wengi hutumia kuogea yaani malapa na ndala hazina hadhi ya sandols Anyway wacha nami niite sandals tu sababu nia yangu ni kuzingumzia hizi sandols ambazo zimemwagika kibao madukani yaani ni toleo jipya kwa kina dada sasa wanazivaa sehemu yoyote ile , yaani imepewa hadhi ya kiatu cha kufunika ambavyo wengine wanadiriki kutokea out au kuvalia hata na suti mradi tu iwe na turangi twa kumechisha na nguo,pochi au hata mapambo. Kwa mtaji huo tunaweza ona shanga zinavyopata deal na wale wanaouza viatu vya sandols vyenye shanga wanasema hivyo ndivyo vina deal kwa sasa mradi tu upangilie rangi vizuri. Madesigner kama LV, Gucci,burberry nawengineo kibao nao hawako nyuma wameshazimwaga sokoni sandals zikiwa zimerembwa kwa rangi tofauti na urembo wa vito vya kung’aa (stones)pamoja na chata zao...kama kawa Enzi hizo viatu kama hivyo vilikuwa vya kushindia nyumbani au kuendea dukani (kuwepo around) lakini sasa watu wanapuyangia town na kutinga navyo hata kwenye mtoko wa maana kama hawana akili nzuri Si unajua kuna hotel au club fulani haziruhusu kuingia na sandals, lakini kwa sasa wamechemsha kwani ndio viatu vyenyewe vya kuulambia kwa kina dada, si wajua huwezi bishana na fasheni kama huizimii unaipisha inapita lakini inakuwa ipo ipo tu!!

Thursday, 29 March 2007
Phatfarm Wanakandamiza!
Pichani ni simple raba inayotengenezwa na Brand ya Phatfarm.....ni raba simple kuivalia aina mbalimbaliza jeanz,pensi kali za jeanz,t-shirt zenye kola alimaarufu kama Form 6 kama tulivyozoea pale bongo,t-shirt za kola ya duwara na zinginevyo ambavyo nimevisahau ila najua wadau wangu ni watu hatari wa kulipuka kwahiyo sina wasiwasi na hapo!Mguu huo unaanzia $80...!

Hata Sanaa Ya Picha Na Mavazi Tupo...Noma DU!
Hao ni watangazi mbalimbali wa redio 88.4 Clouds Fm wakiwa katik mdungo mmoja mkali wa picha.Kusema ukweli hata sanaa hii kwasasa hatuko nyuma kama zamani nadhani unaona hata mavazi waliyovaa simple na yametulia,make up artist wanajitahidi na wametoka nyoko bovu sana......Big Up!

Msisahau Hata Wasanii Wetu Bongo Wamo?
Jamani kama kawaida napenda kutoa shavu pale popote panapohitaji kufanya hivyo,kama pichani ni wasanii wa mashuhuri bongo.....Lady Jaydee na Prof.j wakiwa katika makamuzi flani flani bongo,nadhani wamependeza na wanamziki wengi bongo wanajitahidi sana kulipuka pamba .....au mnasemaje wadau zangu....si wametoka bunduki balaaa?

Spidi 12O Shaaaaaaaaa!Label Balaa Bongo!

Ni lebo mpya ya nguo ndani ya Bongo ambayo wamiliki wameiweka kwenye Hip Hop Gear,wakimaanisha ni mavazi ya kisanii ya Hip Hop. Wamiliki wa lebo hiyo 120 ambao ni kampuni ya 120 Entertainment , ambao pia wanaandaa event,wana Boze Cruz, pamoja na kupromote wasanii. Akiongelea pamba hizo ambazo wasanii pamoja na wazalendo kibao wanatinga, mkurugenzi wa Kampuni hiyo Dagma Iddi alisema si pamba tu bali kuna stika za kwenye magari pia.

...kuna tops, t-shirt na suruali t- shirt na kila aina ya kunguo pamoja na kofia zitakuja hv karibun ....alisema Dagma na kusema bei za pamba zao ni bei poa yeyote anaweza vaa akipenda. malighafi wananunua Asia na china then wanazitengeneza katika kiwanda kilichopo jijini pamoja nakuweka lebo yao ya 120.....speed 120 ya gari na wenyewe wanakwambia ndo speed ya maisha kila mtu atakiwe aende mwendo huo wa maisha kuna wapenzi wa DHW ambao wako nje ya nchi tayari wameanza kuagiza stika na hizi pamba kutoka kwa marafiki na ndugu zao wakidai wanaona fahari kutinga lebo ya home, na hii yaonyesha malengo ya vijana hawa kuipanua hii lebo afrika mashariki na kisha dunia nzima itatimia. kama umeizikia wanakwambia cheeki nao dagmar120@hotmail.com
Tuesday, 27 March 2007
Naomba Maoni Hapo....Mhh Hii Noma...Mnaonaje Mlipuko Huo?
Kama kawaida yake mzee mzima Jay-Z analipuka sana pamba kali sana na ni mmoja ya marap mwenye mafanikio sana kati nyanja nyingi lakini pia tusijaribu kusahaua kwamba anashare kwenye kampuni ya ROCAWEAR...kama hapo pichani yuko Beyonce ambaye nae pia ni mlipukaji mzuri tu wa pamba nyepesi....naomba mnipe maoni yenu kuhusu hizo pamba na je mnaona si hatari....hiyo ni classic formal...balaaaaaa!

Shorty Jumpsuit!
Kwa warembo au mabinti wanaojua kujilipua bila kuona aibu kwa kuvaa 2 hii shorty jumpsuit ni kama umemaliza kazi kwasababu kila ulichonacho kitakuwa kimejiweka fresh....inapendeza sana kama ukikandamiza na highhills moja za maana nadhani kwa wale wanaoweza kumudu aina hii ya mavazi ni wachache ila watu kwasasa wanakandamiza bila uoga na culture za kizamani zimeisha kwa wajanja wanaojijua kama mshalipuka na hii style nawapa shavu kinoma....Big Up sana!

Mkeka Nao Unakimbiza!
Pichani ni aina ya classic moka ambayo ubunifu wake umetokana na style ya usukaji ama kwa sisi tunaotoka bongo tunaweza kutamka kama mkeka kutoka na usukwaji wake wenye ubinifu mkubwa....Aina hii ya viatu vingi vyao vinatengenezwa kwa ngozi na pia vinakuwaga handmade shoes,na watu maarufu duniani kwa utengenezaji wa aina hii ya viatu ni Wataliano na ndio maana viatu vingi vitengenezavyo kwa ngozi asilia vinapatikana kutoka Italy na ni maarufu kama ITALIAN SHOES na ni moja ya viatu ghali sana dunia...kama huo mguu hapo juu huwezi kununua chini ya $250-500 na kama Custom Made vinafika mpaka $1000-2000...Haya kuvaa ni gharama

Sina La Kusema......Kazi Kwenu!
Najuaa warembo nitakuwa nawapa wakati mgumu sna wa kutafakari hiyo miguu nayowadondoshea mara kwa mara ila sio kosa langu ila napenda na nyie muweze kujua swala la fashion na style zake zinaelekea wapi,kama hicho kiatu pichani kimetulia sna na kama mjuavyo na rangi zake pia zilivyochanganywa ni kwa ubunifu mkubwa sna....na aina hii ya kiatu vinapendeza sana kuvaliwa kwenye vipensi nyanya.....gaucho ama kaprizi na pia pensi za jeanz vyote vitatoka na vingine vingi mnavyojua warembo ambavyo mimi nitakuwa nimesahau!Na kama unataka kuingia kingi kununua usafiri huo huwa unaanzia kama $50-200 kutegemeana na brandname ya mguu huo....... mmenisoma hapo?

Ful Kujiachia!
Hapo kwa mara nyingine napenda kuwapa shavu nene warembo wa nyumbani kwa kujua kujilipua popote wapatapo upenyo ni si masihara kwani wanajiweza mno mno na kujitambua ni aina gani ya mavazi yanawatoa nyoko na kupendeza popote wapatapo mualiko.Kama hapo pichani ni warembo wa tz wakijinafsi huko mtoni na hapo ni cardiff...uk.Kusema ukweli swala la jeans kwa warembo wengi linawatoa swafi kuonyesha uzuri kila walichonacho kama uonavyo jeanz,vitop blauzi vikali vyeupe na njano,maurembo kibao shingoni na style tofauti za nywele!Malumbo upo hapo?

Bling Bling Zinahitaji Pia!
Milipuko ya vito vya thamani pia ni style na ujue kwamba vinahitajika sana kwa watu wapendao,ila nadhani pia vinategemeana na mtu na mtu ila kwa wale wazee wa Hiphop Style watakubaliana na mimi kuwa uvaaji wa vingarizo hivyo ni vinatisha na vinapendeza sana sana kwenye t-shirt na jeans,raba simple za maana,na mashati kwa wale wanaopenda kuvaa kama wakali wa mamtoni?ila kaa ukijua ukivaa cha ukweli utakubalika sana na vinajulikana kwa mmeremeto wake!

Kumatch!
Kwa wale wafuatiliaji wazuri wa waambiji na hata wanamziki mashuhuri ulimwenguni nadhani itakuwa vigumu sana kuongelea maswala ya uvaaji wa mavazi ya aina mbalimbali na kukubalika bila hata ya kumtaji Mwanamziki Mashuhuri Kanye West kama mlipukaji mzuri tu wa kila aina ya pamba nyepesi kama uonavyo pichani,Nadhani kumatch mavazi kwa wakati mwingine kunahitajika test ya uvaaji kama hapo pichani mzee mzima kajilipua na shati jeupe la mikono mirefu,bodyfit sweater la brown,suruali ya kadet nyeupe,simple raba na pembeni ana kibebea ushindani wa milipuko cha ngozi ya maana!Nadhani uvaaji kama huu unapendeza sana kwa kila mtu ila kunahitajika umatchishaji uliotulia pia!Walipukaji mpo?

Simple Mtoko!
Hii ni spesho kwa warembo wote wanaopenda kulipuka pamba kali na simple wakati wowote,Nadhani kama uonavyo pichani ni mambo ya style za kisasa kabisa za mabinti wapevu wa milipuko ya mavazi na huo ni mfano 2 wa jinsi gani unaweza ukaamua kutoka bomba mbaya hata kuliko Beyonce,yeye amejilipua na office kubwa {miwani} na kijiblauzi simple kenye nakshi kidogo,kaptula white na simple flat sendoz kali za gold.Sasa hapo mmekubali style inazidi kukuwa na watu wanazidi kuvaa simple na kutoka bomba mbaya!Au nimekosea ?

Sunday, 25 March 2007
Scarf!

Mitandio wazungu wanaita ’Scarf ’imechukua nafasi katika mavazi ya sasa ya wanawake hususan wadada wa kileo wanaoenda na wakati. Mitandio hiyo ambayo iko ya aina tofauti mizito mepesi na ya rangi tofauti nayo ina matumizi tofauti kulingana na wakati na mazingira mvaaji aliyokuwepo. Hapa bongo naona imeshachukua nafasi ya kanga na hata masweta kwani warembo wengi hutumia mitandio kujitanda kwenye baridi na wengine hujitanda kwenye misiba na haya kwenye sherehe mfano Kitchen Part. Zaidi ya kutumika hivyo Scarf hujitanda kwa ajili ya show tu, mfano waweza valia sare na nguo ukajitanda shingoni au ukavaa scarf ambayo ina rangi zinazorandana na nguo, viatu au pochi katika tu ya kujiweka smart na mwenye mvuto zaidi. Wapi waweza itundika......shingoni, mkononi ,ukajifunga kichwani au hata ukaegesha kiunoni, begani kokote upendapo ila inategemea na mazingira na ulivyovaa we mwenyewe na haijalishi kama umevaa gauni, skert au hata suruali ya kitambaa au jeans ipo mingi ya rangi tofauti yenye chata za wabunifu maarufu hususan wale wanaodesign nguo za kike. .....unaambiwa kama waogopa kuvaa rangi zaidi ya nyeupe na nyeusi basi vaa scarf yenye rangi kali kwani ni mojawappo ya kukutoa uoga na kuyafanya mavazi yako yawe bomba zaidi......we waonaje hiyooooo imetulia ehhh?

Combat..!
Ile aina ya uvaaji wa makaptula yenye rangi za kijeshi jeshi ni style na pia imekuja kuwa fashion ya aina yake hasahasa kwa sisi vijana wa kisasa .....aina kama ya pensi hilo la kijeshi hupendeza ikivaliwa na simple snickerz....za aina yoyote ila nyeusi ama nyeupe ni rangi poa sana na huku ukishindilia na t-shirt kalia za rangi moja moja na michapisho ya picha kubwa kubwa ama za watu mashuhuri dunia....nadhani ukifanya hivyo mlipoka utakuwa umekamilika kamili kbs kbs!mpo!

Papa!
Hiyo ndio inaitwa papa au pede-zzz kwa wengi wapendavyo kuitapale bongo,ni aina ya viatu kali mno kwa wale wapenzi wa kupenda kujilipua na pamba za kiutu uzima hata na pamba zingine kama jeanz na aina nyingine ambazo kwa aina moja au nyingine ni zinashabiana na huo mguu hapo juu...kwa wale wanaopenda style hii ya mguu kama unapenda kutungu kumbuka inategemeana na material,na muundo wa kiatu hicho...na bei yake inaanzia $150 na kuendelea kwenye nchi za wenzetu!

Kobadhiiiiiiiiiiiiiiiii!
Hilo linaitwa kobadhi,ila ni aina ya kiatu wazi ambacho kinapendeza sana kuvaliwa kwa aina mbalimbali za mavazi kwa nyakati tofauti ila pia kina kanuni zake za uvaaji......na kinapendeza sana sana kuvaliwa katika jeanz na mashati,suruali nyepesi nyepesi au kwa kivupi ni italian style....!nadhani kwa wapenzi wa aina hii ya sendozi wamenipata fresh!!! mpo?

Oldies..................!
Katika swala la mavazi siku hizi si lazima uvaajia au ubunifu wa mavazi uendane na nyakati flani ila inategemeana na style ambayo mtu anaweza kuvaa aina flani ya mavazi na mavazi hayo yanakutoa vipi....kama hapo pichani unamwona mwanandinga mashuhuru dunia David Beckham kama ajulikanavyoa kama msakata kabumbu na vilevile ni mvaaji mzuri sna wa mavazi na model aliyejuu sana!mhh nazani hiyo kofia,miwani,shati la akili ni kama hivyo ila ni balaa....au mnasemaje?

Mazagazaga Shingoni Balaa!
Uvaaji wa mazagazaga shingoni ni moja kati ya milipuko mikali sana katika nyanja mbalimbali hasahasa kwa mabinti na warembo wengi kwa sasa! Ila uvaaji wa mazagazaga siku hizi yanavaliwaga kutegemeana na aina ya mavazi unayotaka kulipuka nayo......kwahiyo warembo msione ni kazi kujilipua na hayo mazagazaga!Nomaaaaaaaaaaaaaa....

Happiness Chipukizi aliyekomaa katika fani!!

Ukizungumzia wabunifu ndani ya Bongo utakuwa umefanya kosa la jinai kama usipolitaja jina la Happiness Chilima mwana dada aliyezaliwa mwaka 1985, jijini Dar es Salaam Wengi humtambulisha kama mbunifu chipukizi kitu ambacho mimi napingana nao kwani katika fani hii yeye ameshakomaa ni kutokana na kuanza fani hii kwa muda mrefu, kiasi kwamba naona wanampunja wanapomuita chipukizi.

Thursday, 22 March 2007
Jamani...Jamani..Mguu Huo?
Kwa wale watunguaji wenzangu wazuri napenda kuwapa umiza kichwa hapo pichani ili ujiulize swali moja wabunifu wanafikiri nini kama hiyo Driving Moc inayotengenezwa na Brox Brand ambacho kwa wale watu wa milipuko nadhani kwa kukiona tu wameshapangia mpaka mavazi rasmi ya kulipuka nacho bila wasiwasi,na wala sina haja ya kuwaeleza zaidi ila ukitaka kutungua mdundo huo unahitaji kuwa na kama box $130 hivi ili upewe na risiti kwamba umekitungua rasmi.....sina la kusema vitendo tu!Aiseee huu mdundo balaa!

Du..... Kimbiza Bovu!
Napenda kumpa shavu mzee mzima wa Hiphop 4eva Tinashe kwa kuweza kulimudu vyema game hili tight hasahasa katika swala zima la milipuko ya pamba simple kali kama hapo pichani juu akiwa amejilipua kama kawaida!Mhh mzee nimekusoma sana na hiyo COnverse,Jeans na T-shirt la Polo nimekukubali.....Big Up Son!
Women's Work!
Hivyo ni viatu simple na vyepesi sna kwa matembezi ya kujiachia popote pale hasahasa mabinti au warembo wengi wanavifagilia sana sana, kwani huwa vinapendeza sna kwa wale wenye miguu size ndogo na hata size kubwa inategemeana lakini!Aina hii ya viatu vinajulikana kama WOMEN'S WORK na vinauzwa kwa bei tofauti kutegemeana na jina la Brand na Style yake.....Kama hicho juu kinatengenezwa na Brand ijulikanayo kama DELMAN na vinauzwa kuanzia $264.99 au tuseme $265.....mmekionaje kiko bomba ?

China Pia Wapo!
Pia katika swala la kupiga pamba classic halipo tu kwa watasha au wauropiani bala hata wabantu wanajilipua safi sana na wanatoka nyoko bovu kuliko hata hao waanzilishaji wa ubunifu huo,kama uonavyo pichani mabinti na wadau zangu wakubwa Joy na Frida walioko pale China wakikandamiza mtabu kwa kwenda mbele na pia hawajisahau katika swala la mlipuko wa kutisha wa wabunifu mbalimbali kama uonavyo pichani....kusema ukweli nimewakubali...tulieni hapohapo wala msijiguse!e he ehe

Warembo,Mabinti,Visura Ughaibuni!
Kama kawa mabinti na warembo zetu wa kitanzania hawana mzaha hasahasa wanapokuwa nchi za watu,hawalegezi kamba hata kidogo kama uonavyo pichani pamba walizolipuka nazo hapo ni balaa na kusema ukweli mnappendeza na mtaendelea kupendeza kwakuwa mnajua kutungua vyema....nawapa shavu kwa hilo sana tu! Mhhh kimbiza bovu!

Tattoo Ni Fashion!

Ili michoro ambayo huchorwa kwa mwili alimaarufu kama Tattoo imerudi tna kwenye soko na tofauti na dhana ya wazee wa zamani kwamba ni uhuni imepotea na kuwa fashion style siku hizi,na kusema ukweli huwa unawapendeza sana mabinti kuchora sehemu mbalimbali za mwilini!Kusema ukweli mnatoka bomba kinoma,Haya wenye kujiamini jilipueni mabinti....au sio mnaonaje hapo?imetulia ehhh?
Wednesday, 21 March 2007
India Fashion Week 07!

Hayo ndio baadhi tu ya mambo ambayo yanaendelea kujiri au kumiminika katika LAKME' FASHION WEEK 07 ambapo kila mbunifu wa udosini anajitahidi kuonesha mbwembwe zake katika ubunifu wa mavazi kama kijivazi mnachokiona hapo pichani.....nadhani warembo mnaona ni jinsi gani hawa wabunifuni wa udosini wanavyojua kuanda mashambulizi!warembo mpo?
Lime!

Lime ndo ndimu jamani, sasa ipo rangi ya ndimu haswaa ile ndimu ambayo haijaiva ndo rangi ambayo imetufungulia mwaka huu katika rangi kama ilivyokuwa rangi pink mwaka jana. Najua utakuwa umepishana wajanja wameitinga au kuona madukani vitu viingi vikiwa vimegubikwa na hii rangi kama pochi, tops, heren, sketi , skafu na viatu pamoja na pamba kibao za kike na mashati pia ya kiume. Rangi hii nakumbuka enzi silee nipo shule ya msingi ilikujaga lakini tulikuwa tunaziita crazt color kutokana na mng’ao wake, na zilikuwa rangi mbili kama ilivyo lime na hii rangi ya machungwa maarufu kwa sasa kama Bambucha!! Haya mabinti ili ufanane na mjanja na uende na wakati huna budi ya kusaka kivazi kama sio viatu , pochi au chochote upendacho ili kabati lako lifanane na wenzio wanaoenda na fashion. Hata wewe kaisake mtu wangu!!

Mdundoooooooo!

Kwa mabinti nadhani hapo nimewafisha bila hata wasiwasi na mmeshanielewa huo mdundo pichani unatakiwa kulipukiwa na mavazi gani na kwa kujua ni unatisha mtakubaliana na mimi kwamba ubunifu wake ni balaa na kwa binti au mabinti watakaolipuka nao lazima uweke attention kidogo unapoamua......! Uongo?

Mguu Huo!!!!
Nadhani wadau zangu mtakuwa mmekubaliana na mimi % kutokana na mikwaju mikali nayowapa ili wadau zangu mpate sio tu style ila chaguo kama umefikia muafaka wakutaka kutungua,hicho ni kiatu kimetengenezwa na brand inaitwa Michael Kors na ukitaka kuingia bei kinaanzia $150 na kinapatikana ktk rangi mbalimbali pia,je mnasemaje ?Kinatisha!

Mabinti Wakila Bata Mtoni......!
Kama kawaida ya mabinti ama warembo wa kibongo wanajua sana kutumia nafasi zao pale wanapodhuru mabash mbalimbali huko mbele,kama pichani mabinti wanaonekana wakiwa wanakula ful shangwe na kulipuka na pamba kali na za maana bila mchezo....kusema kweli hapo tu ndipo nawapa salute kwa kazi yao nzuri ya kupeperusha bendera unyamwezini!Nadhini kama unatadhimini fresh hizo pamba ni simple lakini ni kimbiza bovu.......mpo waungwana?

Kimbiza Bovu!
Wadau wangu kama mjuavyo na muonavyo hapo pichani ni jinsi tu watu wanavyojilipua kwa catalogue tofauti na kukimbiza bovu,si lazima uige ila inapobidi lazima ufanye hivyo,kama pichani ni Mwanamziki Maarufu Usher akiwa ametoka kwenye bash moja la mastar huko mbele akiwa kajilipua na black adidas,jeanz fedout,shati jeupe ndani na sweater jeusi na kukandamiza au kushindilia na miwani juu oversize...jamani msijifikirie ni balaa tupu !!!!

India Fashion Week 07!
Hayo ndio mambo yaliyojiri hivi majuzi udosini kwenye wiki ya maonyesho ya mavazi mbalimbali kutoka kwa wabunifu mbalimbali udosini ijulikanayo kama LAKME' FASHION WEEK 07 yanayoanyika kila mwaka katika mji wa Bombay au Mumbai! Si utani wahindi wanajitahidi sana kwenye maswala ya ubunifu wako mbele kinoma.....unaonaje ubunifu mlipuko hapo juu?

Tuesday, 20 March 2007
Jumba.....!

Kwenye swala la majumba alimaarufu kama suti hapo nadhani nimewapa mlipuko wa maana
kama uonavyo pichana siku hizi suti si lazima sana iwe na rangi au kitambaa kiwe cha rangi moja bali hata nakshi au uchanganyaji wa rangi uwe wa ubunifu kweli kweli kama hapo pichani mzee mzima Will Smith akiwa kajilipuona na suti hiyo ya kama udongo udongo ama dark gold silk flani na mistari kwa mbali na shati la zambarau na tai ya silk zambarau na kitamba cha silk kifuani si masihara?mlipuko uko nyoko kinoma....mnasemaje?
Sarees .........!
Sarees ni vazi la asili ya kihindi ambalo ni vazi la taifa kwa wahindi wowote duniani!Na kama uonavyo pichani hiyo ni Designer Sarees ni maarufu sana kwasasa,na aina hii ya sarees madhubuti kwa kutokea mitoko mbalimbali,kwajili ya harusi au kwendea kwenye harusi pia.Gharama za sarees zinatofautiana bei kutegeana na materials tofauti au nakshi kwasababu kuna mpaka sarees zinazotengenezwa kwa nyuzi za dhahabu,silver au kuweka mpaka vito vya thamani vilevile.....mambo ya udosini hayo!

Rasta Balaa....!
Mitindo wa nywele aina ya rasta ni mtindo au style ya nywele iliyoko dunia longtime,Style hii inampendeza karibia kila mtu anayependa kuzifuga ila vilevile zinahitaji moyo sana kuzipa matunzo na gharama kwa kiasi kati,Hapo pichani ni mwanamziki maarufu dunia Ziggy Marley ambaye ni mtoto wa Mfalme wa Reggae Bob Marley...Kwahiyo kwa mtu yoyote anayependa aina au style hii ya nywele usisite kujilipua nayo iko bomba kinoma....ohhh

Malu..........................!
Napenda kuwapa shavu nene wadau wangu wa Cardiff.Uk kwa kunirushia hii stock kali wakiwa katika mtoko mmoja mkali sana wakiambatana na pamba kali kama uonavyo pichani kwa jinsi walivyojilipua simple sana,Juu shoto ni malumbo au malu na masela zake akiwa amesongwa mbele na mabinti wakali kutoka shoto neema,viv...Big Up

Mkwaju!

Pichani ni aina ya kiatu ni kama moka ila muundo wake uko tofauti kdg,ila aina hizi za viatu ni poa sana kujilipua navyo kwenye mavazi ya kiofisi au maswala ya jeanz,kodrai,kadet khaki,ila juu inategemeana lakini ukipiga na mashati ya maana yenye mikono mirefu na ukijichapa na cufflinks inatoka shwari!haya wadau kiatu kama hichi kwakuwa kimeshehena ngozi OG basi bei yake kinaanzia $250-350na pia inategemeana na brand ya kiatu hicho ndivyo bei zinatofautiana.

Jaribuni Vimerudi!
Hivi ni aina ya viatu ambavyo ni virefu kiasi chake ila kwa mabinti waliozoea kuvaaga mchuchumio hapo haitakuwa kazi sana kupata control ya kuvimudu hivi viatu!Tofauti yake hivi viatu na mchuchumio ni kwamba aina hii ya viatu pichani vina soli nene na pana sana.Uvaaji wa viatu hivi unapendezea sna kwenye majeans,minisketi,pensi nyanya.....gaucho....kapri inatoka bunduki kinoma!mabinti mpo?

Subscribe to:
Posts (Atom)